UHOLANZI tayari imefuzu 16 Bora ya Kombe la Dunia kufuatia ushindi wa 3-2 dhidi ya Australia katika mchezo mgumu wa Kundi B Uwanja wa Beira-Rio mjini Porto Alegre nchini Brazil. Ushindi huo, unaifanya timu ya Louis van Gaal itimize ponti sita baada ya mechi mbili na kupaa kileleni mwa kundi hilo, ikiwa na mabao nane ya kufunga na matatu ya kufungwa.
Mabao
ya Uholanzi yamefungwa na Arjen Robben dakika ya 20, Robin Van Persie
dakika ya 58 na Memphis Depay dakika ya 68, wakati mabao ya Australia
yamefungwa na Tim Cahill dakika ya 21 na Mike Jedinak dakika ya 54 kwa
penalti.
Uholanzi: Cillessen, Martins Indi/Depay 45, Vlaar, De Vrij, Janmaat, De Jong, Blind, De Guzman/Wijnaldum dk78, Sneijder, Van Persie/Lens dk87 na Robben.
No comments:
Post a Comment