tuwasiliane

Saturday, June 21, 2014

UFARANSA YAIPIGA SWITZERLAND 5-2,NA KUTINGA 16 BORA



Ufaransa imejikatia tikiti ya kusonga mbele ikiongoza kundi E licha ya kuwa na mechi moja imesalia dhidi ya Equador .
Switzerland imebakia ya pili ikiwa na alama tatu na hivyo hainabudi kushinda mechi yao ijayo dhidi ya honduras kujihakikishia nafasi katika 16 bora.

Timu hiyo ya Ufaransa iliyoishinda Honduras 3-0, katika mechi yao ya ufunguzi, iliiangamiza timu ya Uswisi iliyokua na sifa ya kutoshindwa katika michuano kumi, ya kombe la dunia.
Olivier Giroud alifunga bao la kwanza kwa kichwa katika dakika ya kumi na saba naye Blaise Matuidi akafunga la pili sekunde chache baadaye
Karim Benzema alipewa penalti lakini mkwaju wake ukazuiwa na kipa wa Uswisi, Diego Benaglio.
Yohan Cabaye aliurudisha mpira baada ya kuokolewa na Benaglio, ila uligonga juu ya lango la Uswisi.
Ufaransa waliongeza bao la tatu kabla ya muda wa mapumziko.

Olivier Giroud alimpa Mathieu Valbuena pasi safi baada ya kona ya waswisi.
Valbuena hakupoteza nafasi hiyo na akautia mpira kwenye wavu wa timu ya Uswisi.
Katika dakika ya 67, Benzema alikosoa kosa lake la kutofunga penalti kwa kufunga bao lingine baada ya kupokea pasi kutoka kwa Paul Pogba.
Hilo likawa bao la nne bila jibu kwa timu ya Ufaransa.
Kisha Benzema akachangia katika kufunga la tano kwa kumpa Moussa Sissoko pasi ambayo Sissoko alitia wavuni.
Katika dakika za mwisho, timu ya Uswisi ilifanikiwa kupata mabao ya kufutia chozi hata ingawa hayakua na uwezo wa kurekebisha matokeo ya mchuano huo.Blerim Dzemaili alipiga mkwaju wa adhabu uliopita safu ya ngome ya Les Bleusna kuingia


TIMU ya Taifa ya Ufaransa imeitandika Uswisi mabao 5-2 usiku huu na kufuzu hatua ya 16 ya michauno ya kombe la dunia kutoka kundi E.
Karim Benzema amefunga goli kali dakika ya mwisho, lakini kwa bahati mbaya mwamuzi alikuwa ameshapuliza kipyenga kumaliza mchezo huo.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2411#sthash.a9ZhmQI7.dpuf

No comments:

Post a Comment