tuwasiliane

Thursday, June 26, 2014

UFARANSA KUIKABILI NIGERIA KWENYE 16 BORA

Ufaransa ilikamilisha mechi za makundi kwa sare tasa dhidi ya Ecuador.
Licha ya sare hiyo Ufaransa ilisalia kileleni mwa kundi E ikiwa na alama 7 moja zaidi ya Switzerland iliyoisakama Iran katika mechi ya mwisho.
Les Blues walifuzu katika raundi ya 16 bora ambapo sasa watachuana na Nigeria .

Mechi hiyo ilishuhudia kadi nyekundu ya nane katika mashindano haya ya kombe la dunia ,nahodha wa Ecuador Antonio Valencia alipofurushwa uwanjani baada ya kumchezea vibaya Lucas Digne.
Hadi kufikia hapo Ecuador ilikuwa imepoteza nafasi nyingi tu za wazi Valencia na Cristhian Noboa wakiboronga mbele ya lango.

Ufaransa kwa upande wao pia walinyimwa mabao mengi na kipa machachari wa Ecuador Alexander Dominguez aliyelazimika kufanya kazi ya ziada usiku kucha .
Equador walihitaji ushindi ili kuendelea mbele lakini walishindwa kuvunja ngome ya Les Bleus na hivyo safari yao Brazil ikafikia kikomo hapo.

Ufaransa sasa itakwaruzana na Nigeria waliomaliza mechi yao ya kundi F kwa kushindwa na Argentina kwa mabao 3-2 siku ya Jumatatu tarehe 30 katika Estadio Di Nationale.
Washindi wa kundi hilo Argentina watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Switzerland Jumanne ijayo katika uga wa Arena De Sao Paulo.No comments:

Post a Comment