tuwasiliane

Monday, June 16, 2014

SONG KUONDOKA NOU CAMP

Song kuondoka Nou Camp,PSG yamgekia Di Maria.
Barcelona wameziambia klabu za Chelsea na Manchester United kwamba zitapaswa kulipa kiasi cha Euro milioni 20 ili kupata saini ya Alex Song.
Song ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon kinachoshiriki michuano ya kombe la dunia,amekuwa ahaha kupata namba kwenye kikosi cha Nou Camp tangu awasili akitokea Arsenal mwaka 2012.Alex Oxlade-Chamberlain anajiandaa kuwa fiti katika mpambano wa Uingereza dhidi ya Uruguay mara baada ya kuwa katika maendeleo mazuri ya kupona jeraha la goti.

Klabu ya Swansea imekataa ofa ya pauni milioni 4 kutoka kwa Sunderland kwaajili ya beki wao wa kati na nahodha,Ashley Williams.

Carlos Vela atabaki katika klabu ya Real Sociedad kwa msimu ujao kufuatia Arsenal kuonyesha kutovutiwa tena na mpango wa kumrudisha mshambuliaji huyo London.

Klabu za Tottenham,Arsenal,Liverpool na Everton zitakosa saini ya Christian Tello kufuatia winga huyo wa Barcelona kujumuishwa kwenye mpango wa kumnyakua kiungo wa Atletico Madrid,Koke

Klabu hio ya Katalani inataka kuhakikisha inapata saini ya Koke ambaye alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu sana msimu uliopita katika kikosi cha Diego Simeone.

Paris Saint Germain wameanzisha mbio za kuwania saini ya kiungo mbunifu wa Real Madrid,Angel Di Maria pamoja na mshambuliaji wa Barcelona,Pedro mara baada ya kukata tamaa ya kumpata Eden Hazard.

No comments:

Post a Comment