Maafisa wa Qatar wanaaminika kupanga mikakati
madhubuti ya kukabiliana na tishio la kupokonywa uenyeji wa kombe la
dunia la mwaka wa Qatar 2022 kufuatia tuhuma za rushwa .
Kamati andalizi ya michezo hiyo sasa inaaminika
kupania kufanya kila iwezalo ikiwemo kufuata mkondo wa kisheria, ikiwa
kura ya kuchagua mwandalizi wa kombe la dunia 2022,itarudiwa.Qatar inakana shutma za hongo.
Hata hivyo hatma yake imo mikononi mwa mchunguzi wa FIFA,Michael Garcia.
Mwanasheria huyo kutoka Marekani anatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake itimiapo Juni 9.
Rais wa Uefa, Michel Platini, aliyeipigia kura Qatari, alisema kuwa atakubali kufanyike kura ya marudio iwapo shutma za ufisadi dhidi ya Qatari zitathibitishwa.
Msimamo wake uko sawa na ule wa makamu wa rais wa Fifa, Jim Boyce aliyesema kuwa hatakuwa na shida yoyote ikiwa ‘makubaliano yatakuwa ni kura ya marudio kufanywa.’
Maafisa wa Qatari wanadai kuwa mtaji wa takriban pauni bilioni 23, mahsusi kwa ajili ya kombe la dunia la 2022, itapotelea mbali iwapo Fifa italipokonya taifa hilo la ghuba haki ya kuandaa michezo hiyo.
No comments:
Post a Comment