tuwasiliane

Sunday, June 15, 2014

IVORY COAST YAITUNGUA 2-1 JAPAN

MABAO ya vichwa ya Wilfried Bony na Gervinho yaliyopishana kwa sekunde 98 yameipa mwanzo mzuri Ivory Coast katika Kombe la Dunia baada ya kuilaza Japan 2-1 katika mchezo wa Kundi C mjini Recife, Brazil.
Tembo hao wa Ivory Coast walimuanzishia benchi Nahodha wake, Didier Drogba lakini ni kuingia kwake ndiko kulikuja sambamba na mabao hayo.
Nyota wa Japan, Keisuke Honda aliifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya 16 kabla ya Ivory Coast kusawazisha kupitiakwa Bony dakika ya 64 na Gervinho kufunga la pili dakika ya 65. Mapema katika mchezo uliotangulia jana wa kundi hilo Colombia iliiaza 3-1 Ugiriki.
Kikosi cha Ivory Coast kilikuwa: Barry, Aurier, Bamba, Zokora, Boka/Djakpa dk75, Tiote, Yaya Toure, Die/Drogba dk62, Gervinho, Bony/Konan dk77 na Kalou.
Japan: Kawashima, Uchida, Morishige, Yoshida, Nagatomo, Yamaguchi, Hasebe/Endo dk53, Okazaki, Honda, Kagawa/Kakitani dk86 na Osako/Okubo dk68.

No comments:

Post a Comment