tuwasiliane

Friday, June 6, 2014

GEBO PETER AFARIKI DUNIA


MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba Scya Dar es Salaam, Gabriel ‘Gebo’ Peter amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, imeelezwa.

Kaka wa marehemu, Peter Tino ametoa taarifa za awali za msiba wa nduguye, akisema amefariki usiku wa kuamkia leo.

Gebo aliyewika Sigara FC ya Chang’ombe, Dar es Salaam kabla ya kutua Simba SC, hadi anafariki alikuwa mdau mkubwa wa klabu ya Manyema Rangers ya Kariakoo.Msiba upo

nyumbani kwao, Vingunguti Dar es Salaam na umoja wa wachezaji wa zamani wa Simba na Yanga unasimamia mchakato mzima wa mazishi kwa pamoja na familia ya marehemu.

No comments:

Post a Comment