KLABU
ya New York City FC imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa
wa Hispania, David Villa kwa mkataba wa miaka mitatu.
Klabu
hiyo kubwa inayomilikiwa na Manchester City na New York Yankees,
imethibitisha katika mtandao wake wa Twita kuwa nyota huyo mwenye miaka
32 ni mchezaji wao mkubwa wa kwanza kumsajili.
Klabu
ilitweet: “Karibu New York City: David Villa (@Guaje7Villa) rasmi
amesaini kama mchezaji wa kwanza mkubwa kusajiliwa na £NYCFC.
£VillatoNYCFC.’
Villa
anakwenda Marekani baada ya kuwasaidia Atletico Madrid kushinda taji
lake la kwanza tangu mwaka 1996 na kufika fainali ya UEFA ambapo
walipoteza dhidi ya Real Madrid.
Nyota
huyo alijiunga na Atletico majira ya kiangazi mwaka 2013 baada ya
kucheza misimu mitatu ya mafanikio katika klabu ya Barcelona, wakati huo
huo aliwahi kuzichezea Valencia, Real Zaragoza and Sporting Gijon.
No comments:
Post a Comment