tuwasiliane

Sunday, June 29, 2014

COLOMBIA YAITOA URUGUAY,SASA KUKUTANA NA BRAZIL ROBO FAINALI

 MABAO ya James Rodriguez katika dakika za 28 na 50 usiku wa kuamkia leo yameiwezesha Colombia kutinga Robo Fainali ya Kombe la Dunia kwa kuifunga Uruguay 2-0.
Sasa, washindi hao wa Kundi C watakutana na wenyeji Brazil katika Robo Fainali, ambao wameitoa Chile katika mchezo uliotangulia kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120. Rodriguez sasa anakaa mguu sawa katika mbio za kiatu cha dhahabu cha michuano hiyo, akitimiza mabao manne na pia ametoa pasi nne za mabao.

Colombia iliyoongoza Kundi C ilipokuwa pamoja na Ugiriki, Ivory Coast na Japan ilicheza soka maridadi na kuipoteza kabisa Uruguay iliyofuzu kama mshindi wa pili wa Kundi D nyuma ya Costa Rica.

Uruguay ilionekana wazi kuathiriwa na kumkosa mshambuliaji wake tegemeo, Luis Suarez aliyefungiwa mechi tisa za kimataifa na miezi minne kwa ujumla kutojihusisha kabisa na soka, baada ya kumng’ata begani beki wa Italia Giorgio Chillaini katika mchezo wa mwisho wa Kundi D.
Kikosi cha Colombia kilikuwa: Ospina, Zuniga, Zapata, Yepes, Armero, Aguilar, Sanchez Moreno, Cuadrado/Guarin dk81, Rodriguez/Ramos dk85, Martinez na Gutierrez/Mejia dk68.
Uruguay: Muslera, Maxi Pereira, Gimenez, Godin, Caceres, Pereira/Ramirez dk53, Gonzalez/Hernandez dk67, Arevalo Rios, Rodriguez, Cavani na Forlan/Stuani dk53

No comments:

Post a Comment