tuwasiliane

Saturday, June 21, 2014

ARGENTINA YATINGA 16 BORA,MESSI APIGA BONGE LA BAO

Left behind: Messi finally finds some space on the hour, but can not take advantage after firing wide
ARGENTINA imetinga hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia, baada ya kuilaza Iran bao 1-0 kwa mbinde jioni hii Uwanja wa Mineirao mjini Belo Horizonte, Brazil.
Shukrani kwake Nahodha wa timu hiyo, Lionel Messi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida za mchezo huo, akifumua shuti kutoka umbali wa mita 25.

 Argentina sasa inatimiza pointi sita baada ya mechi mbili na kusonga mbele, ikiwaachia Iran, Nigeria na Bosnia kibarua cha kuwania nafasi ya pili ya kufuzu kutoka kundi hilo. 
Iran waliibana haswa Argentina katika mchezo wa leo na ilibaki kidogo tu wafanikiwe kupata sare, sifa zimuendee kipa wao Haghighi aliyeokoa michomo mingi ya hatari.
 
Kikosi cha Argentina kilikuwa: Romero, Fernandez, Garay, Zabaleta, Rojo, Gago, Mascherano, Di Maria/Biglia dk90, Aguero/Lavezzi dk77, Messi na Higuain/Palacio dk77.
Iran: Haghighi,Haji Safi/Haghighi dk88, Hosseini, Sadeghi, Nekounam, Shojaei/Heydari dk77, Timotian, Montarezi, Ghoochannejad, Dejagah/Jahanbakhsh dk85 na Pooladi.

No comments:

Post a Comment