
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe
Scolari,anatarajiwa kuchunguzwa na polisi kulingana na taarifa kutoka
nchini Ureno licha ya kocha huyo kukanusha madai kuwa alikwepa kulipa
kodi.
Bwana Scolari alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Ureno kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2008. Madai hayo yanaonekana
kuhusishwa na wakati wake alipokuwa nchini humo.Katika taarifa yake bwana Scolari alisema kuwa daima amekuwa akiweka wazi mapato yake kwa idara ya utozaji ushuru katika nchi zote alikofanya kazi.
Madai hayo yanakuja mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa kombe la dunia nchini Brazil.
Mwanasheria mkuu nchini Portugal amethibitisha taarifa za kuchunguzwa kwa Scolari, ingawa hakutoa taarifa zozote.
''Ninajiamini mimi mwenyewe sijafanya uhalifu wowote na nimekuwa nikitangaza mapato yangu. Ikiwa kuna jambo lolote ambalo haliko sawa , sio makosa yangu,'' alisema Scolari.
No comments:
Post a Comment