BAO
pekee la Mbwana Ally Samatta jioni ya leo limeipa ushindi wa kwanza TP
Mazembe katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS
Vita uliofanyika Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Samatta
ambaye DRC ni maarufu kama Sama Goal mbele ya mashabiki wa timu yake,
alifunga bao hilo pekee dakika ya 62 na kuifanya Mazembe ifufue
matumaini ya kutwaa Kombe la tano la michuano hiyo.
AS
Vita ya Lubumbashi, DRC inafungwa kwa mara ya tatu mfululizo msimu huu
na ndugu zao hao, baada ya awali kufungwa katika mechi zote za Ligi Kuu
ya nchi hiyo.
Samatta
alimpisha Jonas Sakuwaha dakika ya 82, wakati mshambuliaji mwingine
Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu alitokea benchi dakika ya 67 kwenda
kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba.
Mazembe
sasa ina pointi tatu sawa na AS Vita iliyoifunga Zamalek 2-1 katika
mchezo wa kwanza wiki ambayo akina Samatta walilala 1-0 mbele ya El
Hilal nchini Sudan.
Matokeo
ya leo yanafanya kila timu katika kundi hilo iwe imefungwa mechi moja
na kushinda mechi moja, baada ya El Hilal pia kufungwa 2-1 na Zamalek
jana.
No comments:
Post a Comment