Aliyekuwa mchezaji mahiri wa timu ya Kagera sugar nafasi ya midfild kwa kipindi cha misimu miwili iliyopita, Zuberi Kasim Dabi amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu ya Ruvu shooting ya Pwani.
Dabi amesaini mkataba huo Ijumaa hii, Mei 9, 2014 katika ofisi za Ruvu shooting zilizoko Mlandizi, Pwani mbele ya uongozi wa timu hiyo ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Kanali Charles Mbuge.
Dabi kabla ya kujiunga na Kagera sugar amewahi pia kuzichezea timu za Villa Squad ya Dar es salaam, Polisi Morogoro ambayo musimu huu imefanikiwa kupanda daraja, kucheza ligi kuu.
Ruvu shooting ipo katika mchakato mkali na mkubwa kukisuka kikosi chake
kwa kusajili wachezaji wenye uwezo kama kocha wake mkuu Tom Olaba
alivyoshauri.
Wakati Ruvu shooting wakisajili wachezaji wa timu kubwa, tayari kikosi hicho kimeivunja timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 na kutangaza kukiunda upya kwa kuwafanyia majaribio wachezaji vijana kati ya Mei 15-28, majaribio ambayo yatafanyika katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi.

No comments:
Post a Comment