
Kaimu Meneja wa Manchester United Ryan Giggs amepata
pigo la kwanza baada ya timu yake kupokea kichapo cha goli moja kutoka
kwa Sunderland siku ya Jumamosi.
Sunderland ambayo ilikuwa inapigania kuepuka kushuka daraja ilionekana kutawala mchezo ambao Emanuel Giaccherini na Fabio Borin walikosa magoli baada mashuti yao kugonga mwamba.
Kipindi cha pili Manchester walikuja juu na kujaribu kusawazisha goli lakini wakakosa umakini wa umaliziaji.
Kwa matokeo hayo Manchester United inaendelea kubaki nafasi ya saba na pointi 60 huku Sunderland wakijihakikishia kutoshuka daraja baada ya kujikusanyia point 35 huku wakiwa wamebakiza michezo miwili.
No comments:
Post a Comment