Shirikisho la Kandanda la Afrika (CAF) limethibitisha
kuwa ni mashabiki 5,000 pekee watakaoruhusiwa kuingia kwenye uwanja wa
Tata Rapahel mjini Kinshasa kwa mechi ya Jumapili ya Ligi ya Mabingwa wa
Afrika kati ya AS Vita na wakinzani wao kutoka Misri Zamalek.
Kiwango cha mashabiki wanaotazamiwa kufika uwanjani kiliafikiwa katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika kundi "A" kati ya chama cha kandanda katika DRC (FECOFA) na maafisa wa usalama.
Hatua hizo zimechukuliwa ili kuepukana na msongamano katika uwanja huo.
Mashabiki waliojisahili na walio na vyeti sahihi vya uanachama watapewa nafasi ya kwanza kuingia uwanjani.
CAF wamesema kuwa mwanachama wa kamati kuu ya FECOFA wakiongozwa na Rais wake Constant Omari, wamekagua vifaa katika uwanja huo ili kuhakikisha kuwa kutakuwepo na usalama.
No comments:
Post a Comment