Brendan Rodgers ametia sahihi kandarasi mpya ya muda mrefu kuwa mkufunzi wa timu ya Liverpool iliyomaliza yapili msimu uliopita.
Rodgers ambaye alichukua usukani mwaka wa 2012
kutoka kwake Kenny Dalglish ameiongoza timu hiyo kushiriki ligi ya
vilabu bingwa baada ya kukosa kushiriki ligi hiyo kwa miaka minne.Raiya huyo wa Ireland mwenye umri wa miaka 41 amesema kuwa anajihisi mwenye bahati kwa fursa hiyo ya kuongeza kandarasi na kusalia katika klabu hiyo.
Liverpool ilimaliza ya pili ikiwa na pointi mbili pekee nyuma ya mabingwa Manchester City katika msimu uliokamilika.
Timu hiyo ambayo imewahi kushinda ligi ya premia mara 18 ilikuwa na nafasi nzuri ya kunyakua taji hilo tena tangu mwaka wa 1990, kabla ya kulazwa mabao 2-0 na Chelsea matokeo yaliyoiruhusu mabingwa wa ligiu kuu ya Uingereza Manchester City kuipiku kileleni.
The Reds walikuwa wakiongoza kwa pointi tano walipoialika Chelsea mnamo tarehe 27 mwezi Aprili, lakini kushindwa kwao kukawafanya kupoteza kasi huku City wakishinda mechi zao zote zilizokuwa zimesalia na kumaliza wa kwanza.
Ijapokuwa taji la premia lilimponyoka Rodgers alitajwa kama mkufunzi wa mwaka na shirikisho la makocha wa ligi.
Mwenye hisa mkuu wa Liverpool John Henry na mwenyekiti Tom Werner, katika ripoti ya pamoja walisema kuwa klabu hiyo ya Anfield ilikuwa yenye ‘bahati sana’ kuwa na Rodgers kwenye usukani.
Mwanabiashara huyo wa Marekani alisema kuwa waliweka Imani yao kwa Rodgers kuweza kufanikisha azma ya klabu hiyo, huku akiongezea kuwa Rodgers ni kiungo muhimu sana kwa kile ambacho umiliki wa klabu hiyo kinajaribu kuafikia uwanjani.
John HenryJohn Henry
Henry alikamilisha ununzi wa Liverpool kwa Euro milioni 300 kutoka kwa mmarekani mwenzake Tom Hicks pamoja na Shirika la Marekani la Mill Financial mwezi Octoba 2010.
No comments:
Post a Comment