Rais Joyce Banda wa Malawi ameamuru kusitishwa mara
moja kwa shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu
wa nchi hiyo ulifanyika jumanne iliyopita.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amearifu kutoka mjini Lilongwe kuwa Dr Banda amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kile alichokiita kuvurugwa kwa mtiririko mzima wa shughuli za upigaji kura,kuhesabu na hata namna ya kusimamia utoaji wa matokeo yake.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Malawi Jaji Mackson Mbendera amesema kuwa anawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kuangalia uwezekano wa amri hiyo ya Rais kutekelezwa na kama haijavunja sheria ya nchi.
chanzo bbc
No comments:
Post a Comment