tuwasiliane

Thursday, May 1, 2014

Atletico na Real Madrid katika fainali

Ni Atletico Madrid na Real Madrid katika fainali
Matumaini ya Chelsea ya Uingereza kufuzu katika fainali yao ya tatu ya kombe la mabingwa barani Ulaya katika kipindi cha miaka sita iligonga mwamba uwanjani Stamford Bridge baada ya Atletico Madrid ya Uhispania kutoka nyuma bao moja kwa nunge katika kipindi cha kwanza na kuilaza the blues mabao matatu kwa moja katika mechi ya mkondo wa pili.
Timu hizo zilikuwa zimetoka sare tasa katika mkondo wa kwanza huko Uhispania.
Vijana wa Jose Mourinho ndio walioweka bayana niya yao mapema katika mechi hii , Fernando Tores alipoiweka Chelsea kifua mbele kunako dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza .
Atletico walijitahidi kutafuta bao la ugenini ilikunusuru ari yao ya kuweka rekodi ya kufuzu kwenye fainali hizo na juhudi zao zilizaa matunda Adrian Lopez alipoisawazishia dakika moja kabla ya mapumziko.
Vijana hao wa Diego Simeoni hawakulegeza kamba, kipa wao Thibaut Courtois ambaye anaichezea Madrid kwa mkopo kutoka Chelsea alifanya kazi ya ziada kumzuia John Terry na David Luiz kufunga bao .
Wimbi baada ya wimbi la mashambulizi ya Atletico yalilegeza safu ya ulinzi ya Chelsea na kuzaa penalti baada ya ya mshambulizi wa camerooon Samuel Etoo kumwangusha Diego Costa .
Ni Atletico Madrid na Real Madrid katika fainali
Atletico Madrid walijipata uongozini baada ya mshambulizi matata Diego costa kucheka na wavu kunako dakika ya 60.
Bao la ushindi lilifungwa na Adran Turan dakika kumi na mbili baadaye na kumhakikishia kocha Diego Simeone, fainali dhidi ya wapinzani wao kutoka mji wa Madrid Uhispania, Real.
Fainali hizo zitachezwa mjini Lisbon Ureno tarehe 21 Mei.
Ushindi huo umeipa Atletico tiketi yao ya kwanza ya fainali hiyo tangu mwaka wa 1972 .
Aidha hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo ambapo timu mbili kutoka mji mmoja zinachuana katika fainali.
Real Madrid ilijikatia tiketi ya fainali hizo baada ya kuwalaza mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich mabao 5-0

No comments:

Post a Comment