
TANZIA! Mwanamuziki Mkongwe nchini Tanzania, Muhidin Gurumo amefariki dunia leo hii majira ya saa nane mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Kwa muda mrefu Mzee Gurumo amekuwa akisumbuliwa na maradhi mpaka siku ya leo alipotangulia mbele ya haki.
Hili ni pengo kubwa katika muziki
wa dansi nchini kwani kwa muda wote wa uhai wake amekuwa akitoa
mchango mkubwa katika kuuendeleza muziki huo.
Kifo cha Gurumo kimewagusa wadau
mbalimbali wanaopenda na wasiopenda muziki kutokana na umaarufu wake
mkubwa aliojingea kupitia kipaji chake kikubwa.
Mtandao huu utaendelea kukupatia taarifa zaidi kadri muda unavyozidi kwenda.
Tafadhali endelea kufuatilia kwasababu timu nzima ipo njiani kueleka nyumbani kwa marehemu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mzee Gurumo mahala pema peponi. Ameni.
No comments:
Post a Comment