MABAO
mawili ya Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ usiku huu yameipeleka Simba
SC Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2014 baada ya kuilaza Chuoni ya
Unguja 2-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kwa
ushindi huo, Simba SC itamenyana na URA ya Uganda katika Nusu Fainali
ya pili keshokutwa Uwanja wa Amaan, Saa 2:00 usiku, baada ya Azam na KCC
zitakazomenyana Saa 10:00 jioni.
Messi
alifunga bao la kwanza dakika ya 47 kwa shuti kali baada ya kukutana na
krosi ya Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka wingi ya kushoto.
Bao
la pili, Messi alifunga dakika ya 59 baada ya kupiga mpira kutokea
pembeni kulia na kuwachanganya mabeki wa Chuoni kisha kuzama nyavuni.
Pamoja na kufunga mabao hayo mawili, Messi alicheza kwa kiwango cha juu hii leo na haikushangaza alipotajwa kuwa mchezaji bora wa mechi baada ya mchezo huo na kuzawadiwa king’amuzi cha Azam TV.
Chuoni walicheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza na kuibana kabisa Simba SC kupata bao, hali iliyoashiria mchezo huo ungekuwa mgumu zaidi kipindi cha pili.
Lakini mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mcroatia wa Simba Zdravko Logarusic mwanzoni tu mwa kipindi cha pili, kuwatoa viungo wa kati Jonas Mkude aliyekuwa anacheza chini na Ramadhani Chombo ‘Redondo’ juu na kuwaingiza Amri Kiemba na Ally Badru, yalibadilisha taswira nzima ya mchezo.
Tangu hapo, Simba SC ilianza kucheza kandanda ya kuwapa raha mashabiki wake kwa kushambulia kwa kasi na haikushangaza ilipopata mabao mawili ndani ya dakika 14 za kipindi cha pili.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/Nassor Masoud ‘Chollo’ dk66, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Donald Mosoti, Joseph Owino, Jonas Mkude/Amri Kiemba dk46, Haruon Chanongo, Ramadhani Chombo ‘Redondo’/Ali Badru dk46, Awadh Juma, Ramadhani Singano ‘Messi’Said Ndemla dk70, Amisi Tambwe/Betram Mombeki dk74.
Chuoni; Ahmed Suleiman, Hussein Rashid/Ramadhani Hamad dk49, Mwinyi Mngwali, Ahmed Salum, Saleh Mohammed, Adam Othman, Shaaban Msafiri, Hamad Makame/Yussuf Mohamed, Amour Kitipwa/Abdulkadir Ibrahim, Ame Amour na Ibrahim Jeba.

No comments:
Post a Comment