tuwasiliane

Friday, December 20, 2013

OKWI KWENYE MAZOEZI YA YANGA

Hatumwi mtoto Dukani: Hiyo ndo kauli iliyotawala vinywani mwa wapenzi, washabiki  na wadau wa soka kuelekea mchezo wa kesho Nani Mtani Jembe dhidi ya Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Yanga SC watakapombana na Simba SC katika dimba la uwanja wa Taifa kesho jumamosi kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Mchezo huo wa kirafiki ambao umeandaliwa na wadhamini wa vilabu vyote viwili kupitia kampuni ya bia ya TBL na kinywaji chake cha Kilimanjaro Premier Lager unatazamiwa kuwa na washabiki wengi kutokana na kuvuta hisia za wapenzi wa soka.
Young Africans SC itaingia uwanjani ikiwa na kikosi kamili kilichokamlika kila idara kufuatia wachezaji waliongezwa kipindi cha dirisha dogo Juma Kaseja, Hassan Dilunga na Emmanuel Okwi kuwa fit kuelekea mchezo huo.
Mara baada ya mazoezi ya leo, kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Ernie Brandts amesema kiufundi ameshamaliza kazi yake na kikubwa anachosubiri ni kufika hiyo kesho ateremshe kikosi chake dimbani kusaka ushindi ambao ndio itakua furaha ya wanachama, wapenzi na washabiki wa timu ya Yanga.
YANGA "DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

No comments:

Post a Comment