Uongozi
wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya
thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha
mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Maamuzi
hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya
Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC
mwishoni mwa wiki.
Hatua
ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama
chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi
ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
Ukitazama
uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka
tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri
mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
Young
Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu
hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu
kupoteza pointi.
Kufuatia
kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea
kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo
ukiwa haujakamilika.
Ikiwa
Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika
kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha
msaidizi Fred Felix “Minziro”.
Ili
kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya
Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya
safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika
tutawajulisha.
Aidha
uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye
ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na
Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
Mwisho
tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo
kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga
kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha
katika mzunguko wa pili wa VPL.
Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.
No comments:
Post a Comment