KOCHA Arsene Wenger amesema kwamba
hajakata tamaa ya kumsaini Luis Suarez licha ya mmiliki wa Liverpool,
John Henry kukataa kumuuza mshambuliaji wake huyo kwa Arsenal.
Ofa ya The Gunners ya Pauni Milioni 40
kwa imepigwa chini kwa Suarez – ambaye amelazimishwa kufanya mazoezi
peke yake kutokana na kulazimisha kuondoka, huku Liverpool ikikana
kusaini naye Mkataba wa kumruhusu kuondoka.
Wenger alikutana na maswali kuhusu suala
hilo wakati Arsenal ilipotua Helsinki mchana wa leokuelekea mchezo wa
kesho wa kirafiki wa kujiandaa na msimu dhidi ya Manchester City.
Utata mtupu: Suala la Luis Suarez kuondoka Liverpool limetawala majira haya ya joto
Alipoulizwa kama kauli ya Henry
itamkatisha tamaa katika jitihada za kumsaini Suarez, kocha wa Arsenal
alisema: "Hapana, kwa sababu tupo katikati ya uhamisho na tunaangalia
uwezekano wa kuimarisha kikosi.
"Sijasoma taarifa yake, lakini ni kwamba
inaweza kufanikiwa au hapana. Tutaendelea kuwa na matumaini pamoja na
ambavyo anafanya. Sina cha kuongeza zaidi ya nilichosema kuhusu uhamisho
wa Suarez. Itafanikiwa, itafanikiwa katika njia za heshima na Liverpool,"alisema.
Bwana Profesa: Wenger yupo Helsinki na timu yake kwa mechi ya kujiandaa na msimu
Wachezaji wa Arsenal wakiwasili Helsinki
Arsene Wenger kulia akiwa na Aaron Ramsey leo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
No comments:
Post a Comment