KLABU
ya Al Markhiya Sports Club ya Doha, Qatar imetuma barua kwa uongozi wa
Simba ukiomba umruhusu kiungo wake Mwinyi Kazimoto kujiunga na timu hiyo
baada ya nyota kufanya vizuri katika majaribia yake hivi karibuni.
Habari
za uhakika zinasema, Kazimoto aliyekwenda Qatar wiki iliyopita kusaka
nafasi ya kucheza soka la kulipwa katika klabu hiyo, ameshafanyiwa
vipimo vyote hivyo kinachotakiwa ni kibali tu kwa ajili ya kuichezea
timu hiyo iliyoasisiwa mwaka 1995 ambayo sasa inayocheza ligi daraja la piliJapo
nyota huyo aliondoka bila idhini ya viongozi wa Simba wala wa
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kutokana na kuondoka nchini akitokea
kambi ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Al Markhiya imeiangukia
Simba kuomba ridhaa yake.
Kiongozi
mmoja wa Simba alikiri kuwepo kwa barua hiyo iliyoandikwa na Mohamed
Abu Ali, lakini wenye mamlaka juu ya uamuzi huo ni viongozi wa juu wa
klabu.
“Kweli
kuna hiyo kitu, lakini siwezi kulizungumzia kwa undani zaidi kwani sina
uamuzi juu ya hili na hasa ikizingatiwa mazingira ambayo mchezaji
mwenyewe aliondoka sasa tuwaachie viongozi wenye mamlaka,”alisema
Hata hivyo hakuna kiongozi yoyote wa juu wa Simba aliyeweza kupatika jana baada ya kutopokea simu zao za viganjani.
Kama
Kazimoto atapata baraka kutoka kwa uongozi wa Simba atakuwa ni miongoni
mwa nyota wa Tanzania wanaopata ulaji wa kutakata kupitia soka la
kulipwa.
No comments:
Post a Comment