tuwasiliane

Sunday, June 2, 2013

TAIFA STARS, SUDAN ZATOKA SULUHU

                   picha ya kikosi cha zaman cha staz


Na Boniface Wambura, Addis Ababa I
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jioni hii imetoka sare ya bila kufungana na Sudan kwenye Uwanja wa Addis Ababa mjini hapa katika mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). 

Taifa Stars ambayo iko Addis Ababa tangu Jumatatu (Mei 27 mwaka huu) imeweka kambi katika hoteli ya Hilton kujiandaa na mchezo wa Kundi C dhidi ya Morocco Juni 8 mjini Marakech kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.

Stars, inayodhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager, katika mchezo wa leo, iliwakosa wachezaji wake wawili nyota, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta ambao walikuwa wanaichezea klabu yao, TP Mazembe ya DRC katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Washambualiji wa Stars akina Khamis Mcha ‘Vialli’, Mrisho Ngasa na Amri Kiemba wakiongozwa na John Bocco walilitia msukosuko mara kwa mara lango la Sudan ambalo lilikuwa chini ya beki wa kati Nadir Eltayeb ambaye alifanya kazi ya ziada dakika ya 72 kuokoa mpira uliokuwa ukielekea wavuni.

Stars katika mechi hiyo iliwakilishwa na Juma Kaseja, Nadir Haroub/Vincent Barnabas, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, John Bocco/Haroun Chanongo, Amri 

Kiemba/Khamis Mcha na Simon Msuva/Athuman Iddi ‘Chuji’. Baada ya mechi hiyo, wachezaji wa Stars wamealikwa chakula cha usiku na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro, ambapo watakutana pia na baadhi ya Watanzania wanaoishi Ethiopia kabla ya kuondoka kesho alfajiri kwenda Morocco kwa kupitia Cairo, Misri ambapo inatarajia kuwasili Casablanca saa 8 mchana.
Kocha Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na kitaimarika zaidi baada ya Samatta na Ulimwengu kujiunga na wenzao kesho huu mjini Marrakech.

No comments:

Post a Comment