SIMBA
SC imeendelea na harakati za ujenzi wa kikosi kipya hatari cha msimu
ujao, baada ya saa mbili zilizopita kukamilisha usajil iwa beki wa kati
wa kimataifa wa Uganda, Samuel Ssenkoomi anayechezea timu ya Mamlaka ya
Mapato Uganda (URA).
Habari
za ndani ambazo chanzo chetu kimezipata kutoka ndani ya Simba, zimesema
kwamba Ssenkoomi amesaini mkataba wa miaka miwili kuchezea Wekundu hao
wa Msimbazi.
Huyo
anakuwa Mganda wa tatu katika kikosi cha Simba SC baada ya kipa, Abbel
Dhaira na kiungo Mussa Mudde na inawezekana hadi wiki ijayo, Wekundu hao
wa Msimbazi wakatimiza idadi ya wachezaji wanne kutoka nchi hiyo, kwani
hivi sasa wako mbioni kuinasa saini ya mshambuliaji hatari mno wa The
Cranes.
Aidha,
beki huyo mwenye nguvu na akili za mpira, anakuwa mchezaji wa tano mpya
kusajiliwa Simba SC kwa ajili ya msimu ujao, baada ya awali kusajiliwa
wachezaji wanne wazawa, kipa Andrew Ntalla kutoka Kagera Sugar, beki
Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Mtibwa Sugar, kiungo Twaha Shekuwe
‘Messi’ kutoka Coastal Union na mshambuliaji Zahor Pazi kutoka Azam FC
aliyekuwa anacheza kwa mkopo JKT Ruvu.
Simba
SC imepania kuboresha kikosi chake ili kurejesha makali yake msimu
ujao, baada ya msimu huu kutoka mikono mitupu, ikivuliwa ubingwa na
kukosa hata nafasi ya pili, ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba
SC ambayo mzunguko wa kwanza ilikuwa chini ya Mserbia, Milovan
Cirkovick na mzunguko wa pili chini ya Mfaransa Patrick Liewig,
imemaliza Ligi Kuu katika nafasi ya tatu nyuma ya Azam na Yanga
mabingwa.
Kocha
Mfaransa Patrick Liewig amepewa mishahara yake ya miezi miwili, Sh.
Milioni 12 aliyokuwa anadai na tiketi ya kurejea kwao moja kwa moja na
Abdallah Athumani Seif, maarufu ‘Kingi Kibadeni’, bila shaka atasaini
mkataba wakati wowote kurithi mikoba.
Liewig sasa atakuwa anadai mshahara wa mwezi mmoja, Mei ambao uko ukingoni yeye akiwa tayari Ufaransa.
Simba
SC pia imewaongezea mikataba wachezaji wake chipukizi kadhaa
iliyowapandisha kutoka kikosi cha pili akiwemo Haruna Chanongo, ambaye
alikuwa anapigiwa hesabu na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.
Simba
sasa inaelekeza nguvu zake katika usajili wa mshambuliaji sambamba na
kusaini mikataba mipya na Nahodha wake Juma Kaseja pamoja na kiungo Amri kiemba

No comments:
Post a Comment