AZAM
FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Simba SC jioni hii
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara.
Matokeo
hayo, yanaiongezea Azam pointi moja na kuwa 47, ikibaki nafasi ya pili,
nyuma ya Yanga yenye pointi 52, wakati SImba inabaki nafasi ya nne kwa
pointi zake 36, nyuma Kagera Sugar yenye pointi 37 nafasi ya tatu.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Orden Mbaga, hadi mapumziko Simba SC ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Chipukizi
Ramadhani Singano ‘Messi’ aliunganishia nyavuni mara zote mbili dakika
ya 10 na 14 pasi muruwa za Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya
kushoto.
Kipre
Tchetche aliifungia Azam kwa penalti dakika ya 29, baada ya Khamis Mcha
‘Vialli’ kuangushwa kwenye eneo la hatari na William Lucian ‘Gallas’.
Refa
Orden Mbaga alimpandisha jukwaani kocha Muingereza wa Azam, Stewart
Hall dakika ya 31 ya kwa kutoa maneno machafu, akilalaimikia uchezeshaji
wa refa huyo.
Kipindi
cha pili, Azam walirejea kwa nguvu kusaka bao la kusawazisha na
wakafanikiwa kutimiza azma yao dakika ya 72 baada ya Humphrey Mieno
kuunganisha shuti la mpira wa adhabu lililopigwa na kiungo Khamis Mcha
‘Vialli’.
Baada ya hapo, timu hizo zilianza kushambuliana kwa zamu na kosakosa kadhaa pande zote mbili.
Katika
mchezo huo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor Masoud
‘Chollo’, Miraj Adam, Mussa Mudde, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Haroun
Chanongo/Edward Christopher, Abdallah Seseme, William Lucian/Mwinyi
Kazimoto, Ramadhani Singano na Mrisho Ngassa/Fliex Sunzu.
Azam
FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins
Atudo, Kipre Balou, Luckson Kakolaki/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk, Salum
Abubakar, John Bocco/Abdi Kassim, Humphrey Mieno/Jabir Aziz na Kipre
Tchetche.
No comments:
Post a Comment