tuwasiliane

Thursday, April 18, 2013

DK BILAL AONGOZA MAZISHI YA BI KIDUDE, DIAMOND ALIKUWEPO HADI MSIKITINI KUSHIRIKI IBADA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.Picha na OMR
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ramadhan Nasib (kulia)'Diamond Plutnum', akiwa ni mmoja kati ya wasanii waliohudhuria katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri, mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao  Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja. Picha na OMR.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude'(picha ndogo juu kushoto), wakati wakiingiza jeneza hilo Msikiti wa Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea kijijini kwa marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana huu. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment