Na Boniface Wambura
WASHAMBULIAJI
wa Taifa Stars, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya
TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), wamewasili nchini
jana usiku na kwenda moja kwa moja kambini.
Ujio
wa washambuliaji hao unafanya idadi ya wachezaji walioripoti kambini
kufikia 20 kati ya 23 walioitwaa baada ya mshambuliaji Khamis Mcha
aliyekuwa na kikosi cha timu yake ya Azam nchini Liberia naye kuripoti
kambini leo asubuhi.
Wachezaji
John Bocco na makipa Mwadini Ally na Aishi Manula ambao pia nao
walikuwa Liberia na timu yao ya Azam wataripoti kambini leo alasiri.
Wachezaji hao ni sehemu ya msafara wa timu ya Azam ambao utakuja na
ndege ya mchana kutokea Nairobi kwa vile ile ya asubuhi waliyotangulia
nayo wenzao kuwa imejaa.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha
Kim Poulsen leo inaendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa. Mazoezi hayo
yataanza saa 9 alasiri.
Wakati
huo huo: Mwamuzi Msaidizi wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Leslie
Liunda ameteuliwa kuwa mtathimini wa waamuzi (referee assessor) kwenye
moja ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Shirikisho
la Soka la Kimataifa (FIFA) limemteua Liunda kutathimini waamuzi kwenye
mechi kati ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Libya
itakayochezwa Jumapili (Machi 24 mwaka huu).
Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Martyrs jijini Kinshasa kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika ya Kati (CAT).
Waamuzi
watakaochezea mechi hiyo William Selorm Agbovi atakayekuwa mwamuzi wa
kati, Malik Alidu Salifu (mwamuzi msaidizi namba moja), David Laryea
(mwamuzi msaidizi namba mbili) na mwamuzi wa mezani (fourth official)
Cecil Amatey Fleischer. Waamuzi wote hao wanatoka Ghana.

No comments:
Post a Comment