tuwasiliane

Wednesday, January 30, 2013

azam yaipumulia yanga


Azam FC jioni hii imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodadom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya Azam katika mchezo huo yametiwa kimiani na Kipre Michael Balou wa Ivory Coast, dakika ya tisa, Mganda, Brian Umony dakika ya 20 na Mkenya Humphrey Mieno dakika ya 46, wakati bao l kufutia machozi la Toto lilifungwa na Selemani Kibuta dakika ya 77.
Ushindi huo, unaifanya Azam ifikishe pointi 30, baada ya kucheza mechi 15, ikizidiwa mbili na Yanga inayoongoza kwa pointi zake 32, ingawa imecheza mechi 14.

No comments:

Post a Comment