MABAO mawili
ya kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ usiku huu yameipa Zanzibar ushindi
wa 2-1 dhidi ya Rwanda, katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge uliofanyika kwenye Uwanja wa
Mandela, Namboole, Kampala.
Kwa ushindi
huo, Zanzibar Heroes imefufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya michuano hii,
ikipanda kileleni mwa Kundi hilo, kwa pointi zake nne, Rwanda ikishuka nafasi
ya pili kwa pointi zake tatu, sawa na Malawi, wakati Eritrea inashika mkia kwa
pointi yake moja.
Vialli
alifunga mabao yake moja kila kipindi, la kwanza dakika ya sita na la pili
dakika ya 61, yote akionyesha yeye ni fundi na mwenye akili na maarifa ya soka
kutokana na kutulia na kumtungua kipa hodari kabisa katika ukanda huu, Jean
Claude Ndoli.
Rwanda
ilipata bao lake kupitia kwa Dadi Birori dakika ya 79, ambaye aliingia uwanjani
dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Tumaine Ntamuhanga.
Mchezo wa
leo kama ulivyokuwa mchezo wa kwanza kati ya Malawi na Eritrea ulitibuliwa na
mvua iliyoharibu mandhari ya Uwanja wa Mandela, hivyo haikuwa wa ufundi zaidi
ya ‘butua butua’.
Nahodha wa
Zanzibar, Nadir Heroub ‘Cannavaro’ alisema baada ya mechi hiyo kwamba wamefuta
makosa yao ya mchezo wa kwanza na sasa Wazanzibari wasubiri Kombe, wakati
Haruna Niyonzima wa Rwanda, alilalamikia Uwanja mbovu leo kuwasababisha kucheza
ovyo.
Katika
mchezo wa leo, kikosi cha Zanzibar kilikuwa; Mwadini Ally, Nassor Masoud ‘Cholo’,
Samir Hajji Nuhu, Aggrey Morris, Nadir Haroub Ali 'Canavaro, Sabri Ali, Khamis
Mcha 'Vialli', Abdulaghan Gulam, Jaku Juma, Seif Abdallah/Adeyom Saleh Ahmed dk88 na Suleiman Kassim ‘Selembe’.
Rwanda; Jean
Claude Ndoli, Emery Bayisenge, Hamdani Bariyanga, Ismail Nshutiyamagara,
Mwemere Ngirishuti/Jean Claude Iranzi dk46, Jean Baptiste Mugiraneza, Haruna
Niyonzima, Jimmy Mbagara, Jerome Sina, Jean D’Amour Uwimana/Fabrice Twagizimana
dk24 na Tumaine Ntamuhanga/Dadi Birori dk66.
No comments:
Post a Comment