MAMIA ya wananchi jana wamefurika
katika kitongoji cha Mabulugu, kijiji cha Lamadi wilayani Busega, mkoani
Simiyu, kwa ajili ya kushuhudia tukio la ajabu la mwanamke mmoja
anayedaiwa kufariki dunia na mwIli wake kuhifadhiwa hospitalini, lakini
baadaye akaonekana usiku akiwa mzima na kuingia ndani ya nyumba yake.
Aidha, umati mkubwa watu pia umefurika
kwenye hospitali ya Mkula, kwa ajili ya kushuhudia mwili unaodaiwa kuwa
wa mwanamke huyo, aliyetambuliwa kwa jina la Ngulima Kilinga (30),
uliokuwa umehifadhiwa hospitalini hapo.
Wakisimulia tukio hilo ndugu wa
mwanamke huyo wakiwemo mume wake Bw. Ngitu Masisanga, pamoja na mama
yake mzazi Mwashi Myeya, wamesema kuwa ndugu yao aliugua ghafula juzi
baada ya kukwama na mfupa wa samaki wakati akila chakula nyumbani kwake.
Wamsema kuwa baadaye alipata homa na
kumpeleka katika hospitali ya Mkula, inayomilikiwa na kanisa la AIC, kwa
ajili ya matibabu, lakini muda mfupi alipoteza maisha.
Wamesema cha kushangaza wakati wamelala
ndani ya nyumba yake na waombolezaji wengine, huku maiti ikiwa
hospitalini ghafula majira ya saa 7:00 usiku, ndugu yao alitokea akiwa
uchi wa mnyama na akiwa mzima na kuanza kuita watoto wake na kisha
akavaa nguo zake na kulala kitandani.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa
wakati akiwa ndani ya nyumba hiyo alivaa nguo zake na kuanza kuanga
picha zake kwenye albamu, na kasha alichukuwa tochi iliyokuwa inawaka na
kuizima, hali iliyowafanya watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo
kutahamaki na kukimbilia nje huku yeye wakimfungia ndani hadi jana
asubuhi.
Mama mzazi wa mwanamke huyo amesema
kuwa huyo ndiye mtoto wake kwani amebahatika kuona alama kwenye uso wake
aliyokuwa nayo kuanzia utotoni.
Muuguzi mkuu wa hospitali ya Mkula Bi.
Cymthia Mugussi, anaelezea jinsi walivyompokea mgonjwa huyo na kwamba
alikuwa na upungufu wa damu.
Hata hvyo wananchi wakiwemo wana nzengo
wa eneo hilo waliendea maiti na kuileta kijijini hapo, ambapo ilikuwa
tayari imebadilika sana kwa kuvimba tumbo kama mtu mwenye mimba na usoni
kuonekana kama mzee tofauti na awali marehemu alipokufa na kuhifadhiwa
hospitalini hapo.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
wanaeleza akiwemo mwenyekiti wa wanazengo pamoja na mwenyekiti wa
kitongoji hicho, Bw. Amos Mapema, ambapo wamesema kuwa tukio hilo la
watu kufa ni la tatu kwa siku za hivi karibuni katika kitongoji hicho.
Aidha, kutokana na hali hiyo wananchi
waliazimia kuwa sasa wanawake ndio wawe wanachimba kabuli wakiwatuhumu
kuwa wao ndio wachawi, ambapo kutokana na tukio hilo la jana walipiga
kura za siri na kumbaini mwanamke mmoja kuwa ndiye aliyeua mwanamke
huyo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 41
alinusurika kipigo baada ya mvua kubwa kunyesha hali iliyowafanya
wananchi kukimbia na kumuacha na maiti hiyo eneo la tukio, ambapo polisi
alipata nafasi ya kumtorosha na kumpeleka katika kituo cha polisi
Lamadi, ambako sasa amehifadhiwa.
Akiwa kaituoni hapo Star Tv inamhoji mtuhumiwa huyo lakini anasema kuwa mesingiziwa kwa sababu ya fitina ya watu kijijini hapo.
Diwani wakata ya Lamadi amesema kuwa hadi
jana saa 4:30 a,subuhi maiti ya mwanamke huyo ilikuwa haijazikwa na
kwamba polisi wameenda eneo la tukio, ili kuwaambia wananchi waizike
katika eneo la serikali na kuongeza kuwa pia mwanamke huyo bado
amefungiwa ndani ya nyumba hiyo akifanyiwa dawa za kienyeji ili arudie
hali yake.
CHANZO STAR TV
No comments:
Post a Comment