Kiungo Simon Msuva aliweza kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano kwa Yanga, huku Haruna Moshi 'Boban' akijihesabia ni mwenye bahati kubaki dimbani dakika chache tangu aingie kuchukua nafasi ya Jonas Mkude pale alipoonekana kumkanyaga kwenye goti beki wa Yanga, Kelvin Yondani, ambaye alibebwa kwa machela na hakurudi uwanjani kutokana na jeraha hilo. Mwamuzi Mathew Akrama alimwonyesha kadi ya njano.
Watoto wa Jangwani 'Yanga' wameshindwa kulipa kisasi cha magoli 5-0, kwenye mechi ambayo walimaliza wakiwa 10 huku goli la penati likiwapa sare ya 1-1 dhidi ya Simba iliyowika ndani ya Uwanja wa Taifa hapa Jijini jana.
Mbele ya mashabiki 59,000 kwa mujibu wa takwimu za kituo cha Supersport kilichorusha kwa mara ya kwanza leo mechi ya ligi kuu baina ya mahasimu hao.
Watoto wa Msimbazi 'Simba' walianza mechi vizuri zaidi na wakapata goli zuri la kuongoza ndani ya dakika ya 4 tu kupitia kwa kiungo wa zamani wa Yanga, Amri Kiemba kufuatia krosi safi ya Mwinyi Kazimoto.
Ndani ya dakika za mwisho, Simba waliendelea kutawala huku wakifikisha asilimi 59 dhidi ya 41 za kumiliki mpira.
Muda huo huo Wekundu wa Msimbazi walikuwa wakionana kwa pasi fupi fupi za haraka na walitawala eneo la kiungo na wangeweza kupata magoli zaidi.
Baadaye Yanga walionekana kutulia na kuanza kutawala "possession" huku kioo cha Supersport kikionyesha asilimia 69 kwa Yanga dhidi ya 31 za Simba.
Mbuyu Twite, ambaye alizigombanisha timu hizo mbili kwa kusaini Simba kabla ya kubadili msimamo na kujiunga na Yanga, alikaribia kuifungia Yanga goli la kusawazisha lakini bahati ilikuwa kwa Wekundu wa Msimbazi kwani shuti lake kali liligonga ‘besela’ na kurudi uwanjani katika dakika ya 31.
Naye Kocha mpya wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts, ambaye alikuwa akiiongoza klabu hiyo kwa mara ya kwanza leo, aligundua udhaifu katika dimba la kati lililokuwa likitawaliwa na viungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto, Kiemba na Jonas Mkude. Akamtoa mshambuliaji Hamis Kiiza ambaye alionekana kupwaya na akionekana ana maumivu na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Frank Domayo katika dakika ya 35, ambaye aliingia kujaza eneo la kati pamoja na Athumani Idd 'Chuji', Haruna Niyonzima na Nizar Khalfani.
Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, alichukuwa jukumu la kuangalua usalama wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ulokuwa ukichezwa jana ndani ya Uwanja wa Taifa hapa Jijini kati ya Simba na Yanga.
No comments:
Post a Comment