tuwasiliane

Monday, October 15, 2012

Senegal tayari kwa adhabu

Meneja wa timu ya taifa ya soka nchini Senegal Ferdinand Coly, amesema kuwa wanajiandaa kwa hali ngumu wakati wakisubiri adhabu watakayowekewa kufuatia vurugu lililosababishwa na mashabiki wa timu hiyo siku ya Jumapili wakati wa mechi yao dhidi ya Ivory Coast.

Mechi ya kufuzu kwa kombe la mataifa bingwa barani Afrika kati ya Senegal an ivory Coast ilisitishwa baada ya mashabiki wa soka kuzua ghasia wakati wa mechi hiyo mjini Dakar.
Ivory Coast ilikuwa inaongoza kwa mabao mawili kwa nunge wakati mechi ilipositishwa.

''Tunajiandaa kwa hali ngumu lakini Senegal iko tayari kwa vikwazo.'' alisema meneja Coly
''Kwa wachezaji, lilikuwa jambo la kushtua hasa kwa wale ambao hawajabobea bado.'' aliongeza Coly
Mashabiki hao wa Senegal, waliwasha moto na kuanza kurusha mawe uwanjani wakati Ivory Coast, ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili kwa bila, matokeo ambayo yangeliondoa timu hiyo kwa fainali hizo zitakazo anadaliwa nchini Afrika Kusini.

Mashabiki wa Ivory coast, walilazimika kuingia uwanjani ili kukwepa ghasia hizo.
''Lazima tombe radhi kwa Ivory Coast, na tuhakikishe kuwa tutafanya kila hali kuzuai kutokea kwa ghasikama hizi tena.'' alisema Coly
''Ninahisi huzuni sana kwa sababu jambo kama hili haliruhusiwin kutokea katika uwanja wa mpira kokote''
Wachezaji na mashabiki hao wa Ivory Coast walizindikizwa na maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia ambao walirusha vitoa machozi ili kuwatawanya mashabiki wa Senegal.

Ripoti zinasema watu kumi akiwemo waziri wa michezo wa Senegal, Hadhi Malick Gakou, walijeruhiwa kwenye rabsha hizo zilizotokea katika uwanja wa Stade Leopold Sedar Senghor.

Ghasia hizo zilianza wakati mshambulizi nyota wa Ivory Coast, Didier Drogba, alipofunga bao lake la pili kupitia mkwaju wa penalti huku dakika kumi na tano pekee zikiwa zimesalia kabla ya mechi hiyo kumalizika.
Shirikisho la soka barani Afrika linganli kuamua kuhusu vikwazo vitakavyowekewa Senegal.

No comments:

Post a Comment