Kwani warembo hao wapo Mikoa ya Kanda ya Kaskazini, kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii hapa nchini pamoja na kujifunza mambo tofauti tofauti.
Si wengine bali ni wale Warembo wanawania taji la Redds Miss Tanzania 2012, siku ya jana walitembelea eneo la Utalii la ufugaji Nyoka la mjini Arusha lijulikanalo kama 'Arusha Snake Park' na waliweza kujionea nyoka wa aina mbalimbali pamoja na Mamba, Kenge, Ndege aina ya Bundi, Tai na Tumbiri.
Pamoja na kujionea Nyoka hao na kucheza nao kwa kuwa vaa shingoni pia warembo hao walipata fursa ya kujifunza juu ya tamaduni za Mila ya Wamaasai na kutembelea vibanda vya urembo wa Kimasai.
No comments:
Post a Comment