tuwasiliane

Saturday, September 29, 2012

Tanzania Live Music kutikisa leo

Silingine bali ni lile Tamasha kubwa la Tanzania Live Music Festival, linalotarajiwa kuwika Septemba 28-29mwakahuu ndani ya Viwanja vya Leaders Club hapa Jijini kuanzia mishale ya saa moja usiku.

Tamasha hilo litahusisha wanamuziki maahiri na bendi mbalimbali kubwa hapa nchini, ni pamoja na Sikinde, Msondo Ngoma, B Band, Mashujaa Musica, Akudo Impact, Fm Academia, Wazee Sugu na nyinginezo.

Naye Mratibu wa tamasha hilo, Edwin Ngere, alisema kwamba tamasha hilo litaanza saa 10:00 jioni hadi majogoo, litakuwa la aina yake ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda.

Mbali na bendi hizo pia kutakuwa na wanamuziki watakaosindikiza burudani hiyo ambao ni pamoja na Khadija Kopa ‘Malkia wa Mipasho’ na Mashauzi Classic iliyo chini ya Isha Mashauzi, ‘Jike la Simba’.

Lengo kubwa la tamasha hilo, ni pamoja na kusaidia chama cha Muziki wa Dansi Nchini (CHAMUDATA) kukiboresha na kuendeleza chama hicho.

Wakati huo viongozi mbalimbali wa bendi, wakiwamo Charles Baba ambaye ni Rais wa Mashujaa, King Kikii wa ‘Wazee Sugu’, Thabit Abdul wa Mashauzi Classic, kila mmoja alijinasibu kufanya kweli.

Naye Balozi wa Tamasha la Muziki wa Dansi nchini, Jacqline Wolper, ambaye pia ni msanii wa filamu, alisema kwa sasa wamepania kukuza muziki wa dansi na kwamba zoezi hilo liendelee siku hadi siku ili muziki huo ukue zaidi.

No comments:

Post a Comment