tuwasiliane

Thursday, September 20, 2012

DUDU BAYA MATATANI MWANZA


MWANAMUZIKI wa kitambo kwenye Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ ameingia matatani akidaiwa kukamatwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Ilemela jijini hapa akituhumiwa kutoa lugha ya matusi.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Dudu Baya alikamatwa Jumamosi ya Septemba 15, mwaka huu, saa 10:00 jioni akiwa kwenye Baa ya Villa City na kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kirumba.
Habari zilidai kuwa, kabla ya kukamatwa, Dudu Baya alikuwa akisakwa na polisi ambapo ilisemekana kuwa alikimbilia nyumbani kwao Kisesa, wilayani Magu na baadaye Nyarugusu mkoani Geita.
Ilifahamika kuwa katika msala huo, Dudu Baya aliwatolea matusi yasiyoandikika gazetini wasanii na watangazaji wa vituo vya redio Passion FM, Philbert Kabago na Ezden Jumanne wa Kiss FM, vyote vya jijini hapa.
Baada ya tukio hilo, msanii huyo alifunguliwa jalada la kesi namba MZN/RB/4349/2012 katika Kituo cha Polisi Kirumba ambapo mwishoni mwa wiki alitiwa mbaroni kabla ya kutoka kwa dhamana akisubiri kupandishwa kizimbani wakati wowote.

SOURCE;www.globalpublisherz.info

No comments:

Post a Comment