tuwasiliane

Tuesday, September 4, 2012

04 AUG.ROONEY KUKALIA BENCHI


HATIMAYE kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekiri kwamba Wayne Rooney anasumbuliwa na uzito na kusema kama asipoupunguza, basi asahau kuhusu kikosi cha kwanza.

Ferguson anafahamu kuwa Rooney akishirikiana na Robin van Persie timu itatwaa vikombe vingi, lakini anadhani nyota huyo wa England anaweza kuharibu mipango yake.

Rooney aliumia na kutoka nje ya uwanja wakati timu yake iliposhinda mabao 3-2 dhidi ya Fulham ambapo Van Persie alifunga bao moja.

Mholanzi Van Persie alifanya vizuri katika mechi ya juzi Jumapili alipofunga mara tatu katika mchezo huo ambao Manchester United ilishinda mabao 4-2 dhidi ya Southampton.

Sasa kocha Ferguson amemwonya Rooney apunguze unene au asahau kikosi.

Rooney aliumia mguu katika mechi dhidi ya Fulham na huenda akaendelea kunenepa kwa kuwa sasa hachezi mpira.

Mchezaji huyo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili kutokana na ukubwa wa tatizo lake.

Ferguson anataka kuona Van Perisie na Rooney wakitengeneza ushirikiano mzuri, lakini kazi hiyo inategemeana na uwezo wa Rooney.

"Wayne si kama Ryan Giggs. Ryan hajawahi kunenepa mno katika maisha yake yote. Wayne ni mvulana mdogo anahitaji mechi nyingi. Ni makini, ana nguvu na mbio," alisema Ferguson.

Lakini kocha huyo huwa anafanya mambo kwa kuangalia historia ya familia ya mchezaji, alimsajili Teddy Sheringham akiwa na umri wa miaka 30 baada ya kufahamu kuwa baba wa mchezaji huyo hakuwa mnene katika umri huo.

Ferguson alimpeleka Rooney katika kambi ya Nike huko Marekani kwa ajili ya kupunguza uzito miaka miwili iliyopita, lakini safari hii amesema kuwa mchezaji huyo atabaki kwenye klabu. Hiyo ni baada ya kugundua unene wake upo katika familia.

"Wayne atabaki katika klabu hii, atatakiwa kupunguza unene. Nadhani atakaa sawa," alisema Ferguson.

No comments:

Post a Comment