
Alisema kwa mara nyingi anapopanga kufanya kitu fulani, lazima anahakikisha analimaliza kwa asilimia mia kwani ameingia mzigoni na wapenzi wa filamu wategemee kuona maajabu kutoka kwenye kampuni hiyo ya kisasa.
Ni yule Nyota wa Filamu Swahiliwood mahiri kwneye sanaa hiyo ya filamu Jaqueline Wolper, kupitia kampuni ya JB Production ameingia ulingoni kwa ajili ya kuandaa filamu zake mwenye sambamba na meneja wake Leah Mwendamseke 'Lamata'.
Kwa kuanza na Kampuni hiyo, tayari imekamilisha kurekodi filamu yao ya Malipo.
Wolper alisema ameingia kwenye fani hiyo ya utayarishaji na kwa kuanza anakuja na filamu ya Malipo, ambayo ni filamu ya kipekee kuanzia hadithi, waigizaji wake wameigiza kwa kiwango kikubwa cha kimataifa.
Katika filamu ya Malipo wameshiriki wasanii wakali na Nyota kama Jaqueline Wolper, Blandina Chagula ‘Johari’, Stanley Msungu ‘Seneta’, Hashim Kambi ‘Ramsey’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’, Mgata, Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo, Slim na wasanii wengine kibao, filamu imeongozwa na Laeh R. Mwendamseke ‘Lamata’
No comments:
Post a Comment