
Alisema ameamua kurejesha koti nyumbani lililokuwa likimbana pindi akiwa ndani ya Bendi ya Mapacha Watatu, na atakianika kibao chake Agosti 31 ndani ya Ukumbi wa Mango Garden.
Alisema ameamua kurudi nyumbani na vitu vipya, ambavyo atavianika hapo Agosti 31, wakati wa utambulisho wa kibao hicho huku akiwaahidi wapenzi wakiwemo na mashabiki wake wa bendi hiyo watapata mambo mazuri.
Si mwingine bali ni yule Mwimbaji mahiri wa muziki wa dansi nchini, Kalala Junior, amerejea kwenye bendi yake ya awali, Twanga Pepeta ‘Kisima cha Burudani’ huku akiahidi kuachia kibao kinachokwenda kwa jina la ‘Nyumbani ni Nyumbani’.
Alisema, amekuja na vitu vipya, ambavyo atavionesha kuanzia Agosti 31, wakati wa utambulisho wa kibao hicho na kuwaahidi wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo, kuwa watapata vitu vizuri zaidi ya awali.
Bendi hiyo ilisema kwamba wamempokea Kalala kwa roho moja na kuwa, Twanga ni chimbuko la watu na hivyo akitoka mtu ni lazima arudi, kutokana na raha na burudani za bendi hiyo.
Kalala amepokelewa kwa mikono miwili, na wanaimani kubwa kwamba watashirikiana naye ipasavyo na wana imani Twanga itazidi kunoga zaidi na zaidi.
No comments:
Post a Comment