tuwasiliane

Saturday, August 18, 2012

18 AUG. SIMBA B WAITANDIKA MTIBWA 4-3 - WABEBA KOMBE LA BANCABC SUPER8

Timu ya soka Simba B ya Dar es salaam leo imefanikiwa kuwa mabingwa wa kwanza wa kombe la BancABC Super8 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mabao 4-3 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa kwenye dimba la taifa jijini Dar es Salaam.

Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuzisalimu nyavu za Mtibwa katika dakika ya 18 kipindi cha kwanza baada ya mshambuliaji wake hatari Edward Christopher, kabla ya Shabaan Kisiga hajasawazisha dakika ya 31.

Mpaka mchezo unaisha kwenye dakika 90 timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 3-3, na hivyo kupelekea timu hizo kuelekea kwenye dakika 120 na ndipo kwenye dakika hizo Simba wakapata bao la ushindi, na mpaka dakika 120 zinakamilika Simba 4-3 Mtibwa.

Kwa usindi huo Simba B imelamba kiasi cha millioni 40 kama zawadi ya mshindi, huku Mtibwa kama washindi wa pili wakitia benki millioni 20. WAKATI HUO HUO Mshambuliaji wa klabu ya Simba B ambaye msimu ataonekana kwenye ligi kuu ya Tanzania bara, Edward Christopher ameibuka mfungaji bora wa michuano ya BancABC Super8 iliyomalizka leo kwa klabu ya Simba B kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mipya.

Edward ambaye kabla ya mchezo wa leo alikuwa na mabao matano, katika mchezo wa fainali ya leo aliweza kufunga hat-trick na kusiadia timu yake kubeba ubingwa huku yeye mwenye akimaliza akiwa na magoli nane na hivyo kutawazwa kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo ambayo ndio imefanyika kwa mara ya kwanza msimu huu.

No comments:

Post a Comment