tuwasiliane

Sunday, July 22, 2012

22 JUL.MILOVAN AWEWESEKA KUKOSEKANA KWA OKWI NA MAREHEM MAFISANGO



Alisema, pengo la nyota hao pamoja na uwepo wa nyota wengi wageni, itachukua muda kiasi kuweza kucheza kitimu, hivyo wapenzi na mashabiki wawe na subira.

Hayo yalisemwa na Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Mserbia Milovan Cirkovic kwamba ubutu wa kikosi chake kwenye michuano ya Kombe la Kagame, unachangiwa na pengo la nyota Emmanuel Okwi na Patrick Mafisango.

Kwani kwa sasa Okwi akiwa nchini Austria kwa majaribio ya kucheza soka ya kulipwa, Mafisango alifariki Mei 17, baada ya kupata ajali ya gari eneo la Keko, hapa Jijini.

Kocha huyo alisema kwamba itachukua muda kupata mbadala wa nyota hao wawili, ambao walikuwa chachu ya mafanikio ya kikosi hicho ndani ya msimu uliopita ikiwemo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Alisema uwepo wa Okwi na Mafisango ndani ya kikosi cha msimu uliopita, ilikuwa chachu ya mafanikio ya timu hiyo, hivyo anachofanya ni kukijenga kikosi upya kwani mwelekeo umeanza kuonekana.

Alisema ubutu huo ndio umeifanya iyumbe kwenye michuano ya Kagame inayoendelea ambapo jana Simba iilikipiga kwenye uwanja wa Taifa dhidi ya Vita Club ya DR Congo; na kutika saere ya goli 1 kwa 1.

Kuhusu pengo la Amir Maftah, Milovan alisema litazibwa na Kigi Makassy huku Salum Kinje aliyekuwa majeruhi ameanza mazoezi na Shomari Kapombe aliyekuwa mgonjwa, amepon

No comments:

Post a Comment