tuwasiliane

Tuesday, July 17, 2012

17 JUL. EXCLUSIVE;URA YATAKA KUSAJILI WAWILI SIMBA SC


KLABU ya URA ya Uganda inataka kusajili wachezaji wawili kutoka Simba, mmoja imesema itatamtaja baadaye, lakini ambaye imeshindwa kujizuia kabisa ni beki Ramadhani Haruna Shamte.

HAPA NDIO KILA KITU inafahamu URA leo wamefanya mazungumzo na Simba SC juu ya kusajili wachezaji wawili wa mabingwa hao wa Tanzania, lakini wakasema mmoja wanahitaji kuendelea kumfuatilia, ila ambaye wamejiridhisha atawafaa ni beki wa kulia, Haruna Shamte.

Shamte ambaye aliwahi kucheza hadi timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amerejea Simba msimu huu, baada ya msimu uliopita kutolewa kwa mkopo Villa Squad iliyoshuka daraja.

Beki huyo, aliyepitia kipindi kigumu msimu uliopita, kuanzia kutemwa kwa sababu tu ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Daring Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), siri ya mafanikio yake ni kutokata tamaa, kujituma na nidhamu.

Kocha wa Villa, Habib Kondo alimsifia Haruna kwamba ni mchezaji mwenye nidhamu na bidii ya mazoezi na akamtabiria mafanikio- na sasa hizi ndizo dalili za mafanikio.
Kwa sasa, kwa Afrika Mashariki na Kati, URA, inayomilikiwa na Mamlaka ya Mapato Uganda, ni moja ya timu zinazolipa vizuri wachezaji wake na zisizoendeshwa kwa ubabaishaji.

No comments:

Post a Comment