
Toka pande za mji kasoro bahari (Morogoro), mongwe Selemani Msindi ‘Afande Sele’, anadondosha tuhuma nzito kwa baadhi ya vituo vya Radio vya jijini Dar es salaam.
Afande anasema haoni sababu yoyote ya kuleta nyimbo zake jijini Dar kwani radio nyingi zimeonyesha kuzidharau nyimbo zake.
Akiendelea na tuhuma hizo alisema redio za Dar zina ubanguzi wa mikoa kwani wasanii wengi wa wanotokea mkoani morogoro kazi zao hazipigwi kwa madai kuwa ni kutoka mikoani.
“Hakuna kipya Dar kwani nyimbo zetu kutoka morogoro hazipigwi na hii inatokana na kutubagua kwa madai kuwa ni wasanii wa kutoka mkoani lakini tunachotaka kusema ni kwamba bado muziki upo na uwezo tunao.” alisema Afande.
No comments:
Post a Comment