tuwasiliane

Saturday, July 7, 2012

07 JUL.Wabunge wa Simba na Yanga kuumana

WABUNGE wa Jamhuri wa Muungano wanaozishabikia Simba na Yanga wataonyesha ubabe leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kumaliza ubishi wa mashabiki wa timu hizo kubwa ambao ni wabunge, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilumbana pale timu hizo zinapoumana.

Pia mchezo huo utasindikizwa na pambano la soka baina ya wasanii wa Bongo Fleva dhidi ya wale wa filamu.

Bila kusahau lile la ndondi ambalo bondia Francis Cheka amepania kuendeleza ubabe wake dhidi ya Japhet Kaseba watakapopanda ulingoni leo Uwanja wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wahabari kuwa walipopigana mara ya kwanza, Kaseba aliokolewa na mashabiki wake kwenye Uwanja wa Uhuru na sasa ajiandae kwa kipigo.

Katika hatua nyingine, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper, ambao ni mahasimu kwenye tasnia ya filamu, wameandaliwa pambano la ndondi ili kumaliza ubish

No comments:

Post a Comment