tuwasiliane

Thursday, July 5, 2012

05 JUL.EXCLUSIVE: EMMANUEL OKWI ASEMA BADO ANA MKTABA NA SIMBA - AKIFELI ITALIA MSIMBAZI NDIO NYUMBANI KWAKE


Wakati sekeseke la usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Simba kutoka Uganda Emmanuel Okwi likizidi kushika kasi, taarifa zikisema amejiunga na mahasimu wao wa Dar Young Africans.

Kutokana na sintofahamu hiyo kuendelea muda mchache uliopita niliongea na mshambuliaji huyo wa Uganda crabes moja kwa moja kutoka Kampala Uganda kuhusu hatma yake ya wapi atakapocheza msimu ujao wa soka.

Okwi alisema: "Shaffih hizo taarifa zinazoenea huko Tanzania kwamba nimesaini kuichezea Yanga sio za kweli kabisa. Ni uongo asilimia 100. Mimi bado mwajiriwa mtiifu wa klabu bingwa ya Tanzania Simba. Naipenda na kuiheshimu timu yangu na nitaendelea kuiheshimu saini yangu iliyopo kwenye mkataba ambao bad ninao na Simba. Sasa nimepewa ruhusa ya kwenda nchini Italia kwenda kufanya taratibu za kujiunga na Parma lakini kama mambo yakiwa ndivyo sivyo then mtaawa Msimbazi ndio nyumbani kwangu. Natarajia kwenda Italia ndani wiki hii kwa sababu sasa hivi ninasubiria viza inayotoka ndani ya siku mbili zijazo," - alimaliza Okwi.
SOURCE; SHAFFIDAUDA

2 comments:

  1. simba inajidanganya kumng'ang'ania okwi,kwani isipomuuza hivi sasa mwakani mkataba utakapomalizika atakwenda yanga bure kabisa akiwa free agent,na simba haitaambulia kitu.kumbukeni kilichowapata Tottenham ambayo haikuambulia kitu katika uhamisho wa sol campbell kwenda kwa wapinzani wao Arsenal baada ya kumaliza mkataba.Hivi kama okwi bado ana mkataba simba kwa nini viongozi wa simba wahangaike hivyo baada ya tetesi za kusajiliwa yanga?MWISHO WA SIKU SI LAZIMA ATAOMBEWA UHAMISHO NA SIMBA WATAKUWA NA DISCRETION YA KUKUBALI AU KUKATAA?MMH HAPA KUNA KITU KINAFICHWA

    ReplyDelete
  2. simba hawawezi kumuuza okwi kwa yanga labda chama lingine, kutakuwa hakukaliki pale msimbazi

    ReplyDelete