Mashabiki wa Simba wanao soma chuo cha kiislamu Morogoro (MUM) wamefanikiwa kulipa kisasi kwa mashabiki wa Yanga wanao soma chuoni hapo.
Katika mchezo uliopita ulishuhudia Yanga wakitoka kifua mbele kwa Simba, lakini leo Mashabiki wa Simba SC hawakurudia makosa na kufanikiwa kuwalaza wapinzani wao goli 3-1.
Mchezo huo uliovuta hisia za wanafunzi na wafanyakazi wa chuoni hapo, na kujaa kila aina ya ishara ya upinzani, ulishuhudia Simba wakiandika goli lao mapema na kuanza kuonyesha dalili ya kuwa mcheyo wa upande mmoja kabla ya Yanga kuamka.
SOURCE; ABOOD MSUNI
No comments:
Post a Comment