tuwasiliane

Sunday, June 17, 2012

17 JUN. KIM;Ushindi ni lazima, japo kibarua kigumu.


Mechi ya leo itapigwa ndani ya Uwanja wa Taifa wa Zimpeto hapo jijini, inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa.

Kwani mechi hiyo ni ile ya Timu ya soka ya Tanzania, Kili Taifa Stars, na siku ya leo inashuka dimbani kuwakabili Msumbiji huku Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen, akisema wana kibarua kigumu.

Mbali na ugumu huo alisema ushindi kwenye mechi hiyo ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za Afrika, ni lazima.

Katika mechi ya kwanza iliyopigwa Februari 29, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

“Msumbiji ni timu nzuri, wanacheza kwa kasi, lakini kila kitu nimekifanyia kazi. Ninaamini tutafanya vizuri, kikubwa ni kufuata maelekezo ya kila tunachopaswa kufanya,” alisema Poulsen.

Naye Nahodha wa Stars, Juma Kaseja alisema ana imani kubwa, wataibuka na ushindi kwani kila mchezaji yuko fiti.

Alisema wanataka ushindi kwani wamejiandaa vilivyo, wanajua Msumbiji ni wazuri, lakini wanafungika.

Naye nyota wa kimataifa anayekipiga TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Samatta, alisema Msumbiji wanastahili heshima yao, lakini wao wanataka kushinda.

Mshindi wa mechi ya leo, atapangiwa kucheza na moja ya timu 16 zilizocheza fainali za Afrika Januari mwaka huu nchini Gabon na Guinea ya Ikweta.

No comments:

Post a Comment