tuwasiliane

Thursday, June 14, 2012

14 JUN.Kutimuliwa Dogo Janja kwafichua makubwa!


Siku moja baada ya Dogo Janja kudaiwa kutimuliwa ndani ya kundi maarufu la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dsm, ukweli kuhusu sakata hilo umechanwa wazi na Dogo Janja mwenyewe.

Akieleza kwa uchungu Dogo Janja anasema tangu atit maguu jijini Dar es Salaam hajawahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku maswala ya msosi, malazi na na ada ya shule zikitolewa na rafiki yake Madee aliyemtaja kwa jina la Abdallah Doka.

Anasema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi ambazo kipato chake ni kuanzia milioni moja lakini aliambulia kulipwa senti kidogo tu isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show.

“Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” ameongea uchungu.

“Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja, Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,” anasema.
Mpaka tunaongea naye asubuhi hii, anasema kadi yake imebakiwa na shilingi 25,000 tu.

Tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi.

Dogo Janja anaeleza kuwa inamuuma sana kwakuwa muziki haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia kimaslahi na hadi leo hii anamalizia kujenga nyumba yake.

“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune.”

Ameendelea kusema kuwa hiyo juzi sasa hadi kufikia Tip Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita kisha kuanza kumpiga.

Alichukua simu yake akaondoka nayo.

Kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka kurudi nyumbani (Arusha) ndicho kimemfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na vyombo vya habari.

“Wanajua nikiongea wataabika sana.”

No comments:

Post a Comment