tuwasiliane

Wednesday, June 6, 2012

06 JUN.Kim:Tunajipanga kuikabili Gambia


Alisema kwamba pamoja na timu yake kufungwa vijana wake walicheza vizuri, kwa sasa hawana budi kusahau ya Ivory Coast na kujipanga ili kuwakabili Gambia.

Kwani hiyo ilikuwa mechi ya kwanza katika kundi la C, lenye pia timu za Morocco na Ghambia katika kuwania tiketi ya Kombe la Dunia la mwaka 2014.

Hayo yalisemwa na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya 'Taifa Stars', Kim Poulsen, amepanga kusaka mikanda ya timu ya Gambia huku akitaka kuwasoma kabla ya kukutana nao katika mechi ya Jumapili.

Na aliyasema hayo jana ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere (DIA), baada ya kuwasili kutoka Ivory Coast ambako timu hiyo ilifungwa 2-0.

Aliongeza na kusema kwamba hawana budi kusaka mkanda wa Gambia dhidi ya Morocco ilipocheza Jumamosi na kutoka sare ya bao 1-1.

Alisema kwa kuwasoma kupitia mkanda, watapata mwanga wa namna ya kuwakabili katika mechi ya Jumapuili kwenye Uwanja wa Taifa, hapa Jijini.

Naye nahodha wa Stars, Juma Kaseja, hakuwa kimya alisema kufungwa na Ivory Coast, ni changamoto kwao ya kujiimarisha zaidi kuelekea mechi ya Jumapili.

Stars wanapaswa kukaza buti kwani wakati wao wakitaka kushinda kufuta machungu ya kufungwa na Ivory Coast, Ghambia watakuwa na kiburi cha sare dhidi ya Morocco.

Kwa sasa timu hiyo ya Taifa Stars iko nafasi ya 145 kwa ubora wa soka, kwa mujibu wa viwango vya soka vya kimataifa, Gambia ni ya 113.

No comments:

Post a Comment